Wednesday, November 16, 2011

THE GADDAFI THEY KILLED


KANALI MUAMMAR GADDAFI

Wende wendako salama, hata tena kuonana
Ulofanyiwa kinyama, na wako mlofaana
Wakakuuza ndarama, wasaliti wa bayana
Machozi yangu moyoni, namwomboleza Gaddafi.

Machozi yangu moyoni, namwombeleza Gaddafi
Hata kama mautini, aloyatenda hayafi
Toka pwani na barani, Afrika alisafi
Wakoloni mamboleo, we Gaddafi buriani.

Wakoloni mamboleo, we Gaddafi buriani
Kwako kafika machweo, ya kesho tafakarini
Walokutendea leo, Uropa wanatendani?
NATO nyie hayawani, Gaddafi mmemtweza.

NATO nyie hayawani, Gaddafi mmemtweza
Kumuwinda viwanjani, kwenye nuru hata giza
Mafuta mlitakani , kumbe yeye kizuiza
Mlokufuru ya haki, Gaddafi mmemaliza.

Mlokufuru ya haki, Gaddafi mmemaliza
Kwa Mola nawashtaki, kwa maswali kuuliza
Mbona mnatudhihaki, uhuru wetu kusoza?
Afrika tambueni, Gaddafi kwetu jabari.

Afrika tambueni, Gaddafi kwetu jabari
Kaskazini kusini, alitufaa amali
Na kidete katetani, mzalendo wa halali
Kwa shairi nakuaga, Kanali Muammar Gaddafi.

Kwa shairi nakuaga, Kanali Muammar Gaddafi
Nikitamani kubwaga, hawa malofa walafi
Tushikaneni mabega, tuwawinde hawa chafi
Nenda wendako salama, Gaddafi Allah Kareem.


IN LOVING MEMORY: COLONEL MUAMMAR GADDAFI
ASSASSINATED BY NATO FORCES AND NTC TRAITORS.
REST IN PEACE.